Neno hili lina maana ya kushikana limetoka katika lugha ya Kichagga katika mkoa wa Kilimanjaro,
Neno hili linaweza kuwa na maana zaidi kwa Kiswahili tushikamane (umoja)
Luwarane ni umoja wa familia ya Temu wanaoshirikiana na kusaidiana katika matukio mbalimbali yakiwa ya shida na raha, pia kupeana ushauri mbalimbali hasa katika Nyanja za kiuchumi na maendeleo. Pia kuwaunganisha wanakikundi cha LUWARANE popote walipo katika Tanzania.
Umoja huu utakuwa na nguvu kwa kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuona mwenendo wa uhai wa kikundi. Waliopewa kipaumbele ni wale wana ukoo wa Temu na ambao wametoa ada na viingilio ili kuboresha utoaji wa huduma zaa kijamii pale inapopaswa.
Umoja huu sio wa kisiasa wala haifungamani na kikundi chochote cha siasa, hivyo ni kikundi huria cha kifamilia na kijamii.
Umoja huu hauendeshwi kwa kuzingatia itikadi za kidini hivyo haifungamani na dini yeyote katika kujiendesha kwake bali wanachama wake tu
Kikundi kitaongozwa kwa kuzingatia kanuni za katiba ya LUWARANE kupata viongozi wake na sio vinginevyo.
No comments:
Post a Comment