HISTORIA YA WACHAGGA MKOA WA
KILIMANJARO
Mkoa wa
Kilimanjaro ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba
25000. Mlima Kilimanjaro, mlima
mrefu kupita yote barani Afrika, umo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Jina
la mlima huu ndilo limeupatia mkoa jina lake.
Mkoa wa Kilimanjaro umepakana na Kenya
upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa kusini na mikoa ya Manyara na Arusha upande wa magharibi. Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia
ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la
Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia
kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki
(Tarakea, Rombo) hadi magharibi
kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).
wachagga
Kabila la Wachaga linafahamika kwa
wengi kuwa linapatikana mkoani Kilimanjaro.Kwa asili, Wachaga ni mchanganyiko
wa Wamasai, Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.
Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya
17.
Walipofika wakiwa katika vikundi vidogovidogo waliwakuta wakazi, wenyeji kwenye
Misitu ya Mlima Kilimanjaro walioitwa ìWakonyingo..
Wenyeji hawa ambao huitwa Mbilikimo hawakupenda kuchanganyika na wahamiaji
wageni, hivyo wakahama na kuanzisha makao yao ya kudumu kwenye misitu minene
iliyopo nchini Kongo.
Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba
wamegawanyika katika himaya 15, wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na
mwonekano wa miili yao.Wachaga wapo katika makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo
na Rombo.
Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha, Wamasama, Wamachame,Wangíuni,
Wakibosho, Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana eneo la Vunjo ni Wakirua,
Wakilema, Wamarangu, Wamamba na Wamwika.
Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati na Wasseri.
Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza
kwamba jina hilo linatokana na neno la Kiswahili linaloitwa 'Kichaka'.
Inaelezwa kwamba misafara ya wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na Waswahili
pamoja na Waarabu, walipokuwa wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji wa
huko wakiwa wamejenga vibanda vya kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama
waharibifu.
Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi vichakani na kuanzia hapo wageni
wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na
waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda kwenye nchi ya ìUchakani,î,
wakimaanisha kwamba kwa watu wanaoishi vichakani.
Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri neno hili na kuliita ìUchagani,
Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa nchi ya ìWachaga.î Hivyo ndivyo
wenyeji waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima Kilimanjaro walivyopewa
jina lao. Wachaga.
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu
wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama
Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika,
Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha ya
Kichagga
Lugha ya Kichagga
inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mlima
Kilimanjaro.
Kutokana na tofauti hizo Kichagga
kimegawanyika katika Kirombo (ambacho nacho kinatofautiana kadiri unavyotoka eneo
moja hadi jingine; mfano Kisseri, Kimashati, Kimkuu, Kimengwe, Kimahida), Kivunjo,
Kimarangu, Kirombo,
Kioldimoshi, Kingassa, Kiuru, Kikibosho, Kimachame
na Kisiha.
Lugha hizo zinakaribia kufanana
kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na
Kioldimoshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia
kinafanana kidogo na Kikibosho.
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu
za Meru,
Arusha,
na kuchanganyikana na Waarusha, hivyo lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru.
Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi
zao zinatofautiana kidogo.
Koo za Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu
gani ya Uchagga, japo si lazima kuwa hivyo: kwa
mfano, familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi,
Mmasy Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame.
Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kamnde, Kileo, Kimambo,
Tesha, Msaki, Assey, Kyara, Kessy, Ndanu, Macha, Mbishi, Kombe, Njau wanatoka
Old Moshi na Vunjo.
Majina mengine ya Old Moshi ni kama yafuatayo: Mmari, Macha, Mshiu, Kyara,
Moshi, Massamu, Kimambo, Mboro, Mlngu, Saule,Tenga, Njau, Malisa, Maro, Maeda,
Ringo,Olomi, Ngowi, Lyatuu na mengine mengi.
Kavishe, Mariki, Tarimo, Laswai,
Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Silayo, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo,
Masue, Maleto, Mramba, Kauki wanatoka Rombo.
Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi,
Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau,Mtei wanatoka Marangu na Kilema.
Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao,
Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso,
Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo,
Mkony, Temba, Foya, Munishi, Kilawe, na kadhalika hutoka Kibosho.
Utawala
wa jadi wa Wachagga
Watawala wa Kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba,
ng'ombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri.
Baadhi ya Ma-mangi mashuhuri katika historia
ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (Wajerumani),
Mangi Sina wa Kibosho na Mangi Horombo wa
Keni - waliojulikana kwa uhodari wao wa vita katika kupigana na
Wamachame na kupora ng'ombe na mazao yao, hata mpaka leo makabila ya Kimachame
na Kikibosho hayaoani kwa urahisi, na Mangi Marealle wa Marangu
na Vunjo. Mangi Meli huyu alikuwa mangi wa waoldmoshi ambaye alipigana na
wajerumani na aliishia kukatwa kichwa na mpaka sasa kichwa chake kipo ujerumani
alizikwa kiwiliwili tuu baada ya kumnyoga na mti aliyonyongewa upo mpaka sasa
sehemu ya Oldmoshi bomani karibu na Kolila Sekondari .
Wakoloni walipokuja Kilimanjaro
waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao
ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa Ma-mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya
kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia
wanaaminika walikuwa kama mabepari wa kwanza wa kijadi, maana walifanyiwa kazi na watu
wengine wakati wao Ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao.
Usemi maarufu wa
"u-Mangi-meza" nadharia inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa Kichagga.
Elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao
mkubwa katika uwanja wa elimu, hususani katika masomo ya sayansi na hisabati.
Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo wamisionari
wa Ukristo
walijenga makanisa
na shule.
Sababu hii imefanya Wachagga kuwa
kabila namba moja lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa (elimu ya
juu) na mkoa
wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari
nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa huo una shule za sekondari
zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi
zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa
mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika
mkoa huu kwa sababu zifuatazo:
1) Hali ya hewa
na vivutio vya kitalii
katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi
na wakoloni
na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza
wakifuatiliwa na serikali za wakoloni
2) Serikali ya Tanzania ilirithi
shule zilizojengwa na wakoloni
3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye
waliwekeza kwenye ujenzi
wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati
wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule.
4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3
utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika
mikoa mingine yote.
Ni vema pia kusema kuwa shule hizo
huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo
kwa watu wote, kwa Wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha
mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi.
Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba".
Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia
yake. Bahati
mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi huko Uchaga ulipelekea Wachagga
wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta Wachagga wakiishi Dodoma,
Morogoro,
Iringa,
Mbeya
n.k. wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula.
Ukienda kwenye mikoa hiyo utakuta
wamejenga jamii
zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe
au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza
kuikuta kwenye makusanyiko ya Wachagga katika mikoa
mbalimbali.
Kilimo na
chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula
kama vile mahindi,
maharagwe,
viazi,
ndizi,
ulezi
na mboga
mbalimbali.Kuna vyakula na mazao ya kienyeji kama vile viazi vikuu, majimbi
“sowe” “shiha”pia matunda ya maparachichi,matimamti,flaumene Matunda posi
Msambochi, ndaraho,ndawiro nk. Pia mazao ya biashara kama
vile kahawa,
nyanya
na vitunguu.
Ndizi za
Wachagga
Ingawa Wachagga wa leo wanakula
vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali
na viazi,
chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.
Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa
matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na
huliwa mbivu kama tunda.
Ndizi mshare,Mrhirhiwe,Mkonosi,
Ndishi,Matoke, Kitarasa hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali
pamoja na nyama
ya ng'ombe,
kondoo
au mbuzi.
Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde,mrhondo, au hata maziwa
ya mtindi.
Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu
na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi ng'ombe (mrharhao,kipungarha
)ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa
kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze
kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa
pamoja na chai
au pombe. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa
sambamba na muhogo
au kuku vumbi au kiti moto.
Maendeleo ya Wachaga
Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la kahawa. Walifanikiwa kuanzisha
vyama vya ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha Halmashauri ya Wachaga
(Chaga Council) ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu ìMshumbue Thomas Marealle II.
Mwaka 1946, utawala wa Waingereza uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga.
Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini
zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo
na Rombo.
Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo
kuwasomesha watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha
Makerere, Uganda.
Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:
1- Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri
ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja
wao.
2- Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye
ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga.
3- Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni
zao lililowaletea maendeleo.
4- Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana
plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi
na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote.
Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila
zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi
Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya kila aina.
5- Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama
kuu ya mamlaka ya Wachaga.
Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi
nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira
chui hawa wametoweka.
Sikukuu ya Wachaga
Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama
kumbukumbu ya siku ambayo Wachagga wote walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu
baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya Uchagga.
Halmashauri hii iliongozwa na Mangi Mkuu ìMshumbue Thomas Marealle II.
Mwaka 1946, utawala wa Waingereza uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga.
Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17 (himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini
zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo
na Rombo.
Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu na huduma za jamii ikiwamo
kuwasomesha watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali kama Chuo Kikuu cha Makerere,
Uganda.
Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera yake ambayo ipo hadi leo kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:
1- Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya bendera ukionyesha mandhari nzuri
ya kilele cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni kielelezo cha umoja
wao.
2- Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto wa bendera kuna mgomba wenye
ndizi. Hiki ni chakula kikuu cha Wachaga.
3- Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni ukiwa na matunda yake. Kahawa ni
zao lililowaletea maendeleo.
4- Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale' lenye matawi mawili (draceana
plant). Matawi haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha Kibo, mgomba wa ndizi
na tawi la zao la kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana na Wachaga wote.
Ni alama ya amani. Masale hutumika katika sherehe na shughuli zote za kimila
zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni kijani kibichi yanayoonyesha jinsi
Kilimanjaro ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya kila aina.
5- Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui ambaye amejipumzisha. Chui ni alama
kuu ya mamlaka ya Wachaga.
Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi
nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu pamoja na uharibifu wa mazingira
chui hawa wametoweka.
HISTORIA YA UKOO
Kutokana na histora inavyojitanabahi
ukoo wa akina Temu ni ukoo wa asili katika kabila la Wacchaga ikiwa asili yao
ni kutoka kwa wakamba
Mila za ukoo bado ni nzuri
kuzingatia maadili tuliyopewa na mababu zetu.
Hapo awali wazee wa ukoo walikuwa ni
wanuwezo mkubwa katika uongozi na waliweza kuchaguliwa kama mchili na kwenye
mabaraza ya mangi, pia walikuwa na maone katika elimu ni miongoni mwa ukoo wenye
wasomi pia ni matajiri wa awali. walikuwa na mali kama za mashamba nyuma kwa
maana kulikuwa na wahunzi (wengine wakapatiwa mchuma) hodari wa ufundi hasa
kutengeneza silaha za kijadi mkuki (iphumu, soka, mndo, chumbuo nk) Wazee
wakotemu walikuwa wafugaji na wafanya biashara za kubadilishana.
Ukoo wetu hutaweza kuona makaburi ya
zamani sana kwani ilikuwa hawaziki bali ilikuwa wanahifandhi katika nyumba ya
nyasi ambayo ilikuwandio nyumba ya asili ndiko mwili ulihifadhiwa na kufunikwa
na mbolea kwa muda wa miaka mitatu na baadae mifupa ilichukuliwa na kuwekwa
mahali maalum ambapo palijulikana kama (mbuwonyi) ni eneo la kuchinjia na
kutole mitambiko mbalimbali kulingana na hitaji. Umoja wa ukoo ulikuwa ni
makini wakotemu walikuwa hawasahauliani wakichinja ni lazima kumuita ndugu au
kumpelekea nyama kuonyesha ishara ya upendo. Pia walialikana kalam kuna msiba
au sherehe utakuta kila mtu anachangia ndizi,mbuzi na nguvu kazi kufanikisha
shughuli hiyo. Ukoo wa Akina Temu ndio ulikuwa na wasomi wa mwanzo wa Kichagga.
Pia katika ujezi yule ndugu ambaye
alionekana mnyonge walialikana na kumchangi ujenzi wa nyumba enzi hizo ni nyasi
hivyo walijipanga wakukata fito,nyasi,wakubeba mawe kwa ajili ya msingi na
(moondi wo umbe na koombe)Ukoo wa temu hauna magonjwa ya kurithi ni watu na
afya zao. Katika ukoo kila mzee wa familia alimtafutia motto wake sehemu ya
kuishi (kiwamba) na ikiwa hakua eneo aliweza kutafuta pengine kwa kununua.
Nyumba hizo za asili kwa sasa
zimekuwa adimu na mahali pa kuweza kuziona ni makumbusho ya vitu vya asili na
utamaduni wake.
Nyumba hii iikuwa na sehemu mbalimbali zilizokuwa zinajulikana kama ifuatavyo:- Kuna koombe –sehemu ya mifugo Kimolya – sehemu ya mbele ya kuhifadhia vitu muhimu sana na hakuruhusiwa watoto kufika huko Kuna Kiwangowangonyi- kuhifadhia panga au mundu Kuna mrwawenyi – kuhifadhia chimbio Kuna moou – sehemu ya malisho ya mifugo Kuna kai – ni dari sehemu ya kuvundikia ndizi Upurhunyi – sehemu ya nyuma ya mifugo ya kutolea mikojo ya ng’ombe na mbuzi Kuna eneo la kichinyi au ulyii eneo la kulala Pia nyuma ya nyumba kwa nje ilijulikana kama Karhii ambapo kma kuna dharura,maongezi ya siri yalifanyikia eneo hili na liliheshimika huwezi kubisha hodi na kwenda moja kwa moja enoe hilo,pia ni sehemu ya kuogea |
Ukoo wa akina Temu kam historia
inayozungumza imegawanyika katika makundi matatu mpaka manne
- Kuna Temu toka Kilema juu karibu na maua
mpaka Ngangu na maeneo chini yake kidogo
- Kuna Temu iliyopo sembeti na ikavuka mpaka
kilema chini maeneo ya masaera
- Kuna Temu iliyopo Mamba, mwika, mpaka Mamsera
NB. UkooTemu iliyopo Babati,Sanya Juu
wote ni wahamiaji lakini asili yao ni kutoka maeneo tajwa hapo juu.Pia kuna
Temu wapo Kenya mmoja alikuwa Anaitwa Naftali
Temu alishinda mbio huko Mexico pia kuna mtangazaji TV nae Temu hivyo utaona historia
inavyozunguka ni baadhi ya babu zetu katika harakati za kutafuta maisha hadi
Kenya.
Ikumbukwe kuwa zamani watoto
waliokuwa wana zaliwa walikuwa wachache pia walikuwa wanashambuliwa na magonjwa
hivyo kujikuta ukoo unakuwa hauongezeki hivyo babau zeu walisafiri kwenda eneo
lingine kuowa na kuongeza familia ndipo Ukoo ukajikuta umetawanyika ingawa
chanjo ni kimoja pia inasadikika kuna wengine walitofautiana mtu na mdogo wake
anahamia sehemu nyingine na kuwanya ukoo kukua na kusambaa.
Imani (dini)
Ukoo wa akina Temu ni ukoo kongwe
hivyo kama inavyojulika walikuwa wasomi wengi wa mababu zetu walishirikiana na
wamissionari waliofika katika maeneo yetu hivyo walijikuta wakiwa katika dini
mbili za awali Lutheran na Roman catholic
Kundi la Ukoo walipitia kilema wengi
wao Roman Catholic walioelekea Mamba na Mwika wengi wao wanasali Lutheran
lakini Temu ya Marangu Sembeti, Kilema chini ni mchanganyiko wa Roman Catholic,Islamic
na Lutheran ingawa imani hizo hazikutengua undugu wa ukoo.
Kuna mila za ukoo ambazo bado
zinafuatutiliwa ili ziwekwe kwenye machapisho ambazo utafiti wake umekamilika
mfano:
Kupokea mtoto aliyezaliwa ndani ya
ukoo
Kuombana msamaha ndugu wakikoseana
Baba na mama wakipigana taratibu za
kurusiana
Kuzaa na mke wa mtu ni kuvunja
heshima ila kuna taratibu
Kuzaa na ndugu kwa bahati mbaya bila
kujuana
Kumtuhumu ndugu kwa kumlaani ndugu
yako /viapo/leka
Taratibu za kuoa ukoo mwingine
Mazishi ya mtu mzima baba/mama/babu
na nk
Mwana ukoo aliyefia mbali na kuzikwa
huko taratibu za kumrudisha nyumbani
Kushikwa ugoni na mke wa mtu
taratibu zake
Utaratibu wa kuarifu ukoo kuhusu
harusi ya mtoto me/ke
By Fulgence Edward Chezamkono Tisira Temu.
No comments:
Post a Comment